Switch to App

Trump akubali kazi ya Elon Musk

Baada ya shangwe na nderemo kutoka kwa umati uliokusanyika, Trump alianza kuzungumza juu ya mtu ambaye amekuwa sehemu muhimu katika kampeni yake – mmiliki wa mtandao wa X na mtu tajiri zaidi duniani Elon Musk.

Alimtaja Musk kama “nyota mpya” wa Chama cha Republican, kabla ya kuendelea kusimulia hadithi ndefu kuhusu jinsi alivyomwacha bilionea huyo akiwa amesimama kwa dakika 40 wakati akitazama video ya roketi ya kampuni ya SpaceX.

Trump Musk anamtaja kama mtu “wa kipekee”.